|
1.
Kosa si kukosa, bali kosa ni kulirudia kosa lakini kila kosa lina
mwisho wake.Thibitisha ukweli wa dhana hii ukirejelea riwaya ya Mwisho
Wa Kosa-Z.Burhani. (Al.20)
2.
Taasubi ya
kiume ni mfano wa kitamaduni ambao umekita mizizi katika jamii ya
mwandishi wa riwaya ya Mwisho Wa Kosa.Thibitisha swala hili ukirejelea
riwaya hii. (Al.20)
3.
Kwa kuzingatia matukio katika tamthilia ya Kifo Kisimani-Kithaka
wa Mberia, fafanua kwa kutolea mifano,nafasi ya mwanamke ukiwarejelea
vijana na wazee. (Al.20)
4.
Maudhui ya utu na wema yametanda kote katika tamthilia ya Kifo
Kisimani.Thibitisha. (Al.20)
5.
Fafanua jinsi maudhui ya usaliti yalivyojitokeza na kuchangiwa na
wahusika katika tamthilia ya Kifo Kisimani. (Al.20)
6.
Umoja na kusaidiana ni jambo la dharura ili kunufaisha na kuleta
maendeleo katika jamii.Kwa kuirejelea riwaya ya Mwisho wa Kosa,tetea
kauli hii. (Al.20)
7.
Mwanamke ni adui ya mwanamke.Kwa kuirejelea hadithi fupi ya
Uteuzi wa Moyoni-Rayya Timmamy,thibitisha ukweli wa kauli hii. (Al.20)
8.
Ukosefu wa elimu unachangia katika uambukizaji wa uwele nduli wa
Ukimwi.Kulingana na hadithi fupi ya Siku ya Mganga-Chesi Mpilipili,tetea
kauli hii.(Al.20)
9.
Pwagu hupata pwaguzi.Kwa kuirejelea hadithi fupi ya Pwaguzi-Amiri
Swaleh, thibisha ukweli wa methali hii.(Al.20)
10.
Maudhui ya utabaka na maendeleo baada ya uhuru nchini Kenya
yamesawirika vyema katika hadithi fupi ya Msamaria Mwema-K.W.
Wamitila.Fafanua.(Al.20)
11.
Kwa kuirejelea hadithi fupi ya Ndimi za Mauti-Timothy M.
Arege,eleza jinsi utukutu wa wanafunzi na uongozi mbaya unavyochangia
katika migogoro na migomo shuleni.(Al.20)
12.
Eleza umuhimu wa mhusika Bi.Keti katika riwaya ya Mwisho wa
Kosa-Z.Burhani.(Al.20)
13.
Uwajibikaji ni jambo la dharura katika jumuiya ya mwandishi wa
riwaya ya Mwisho wa Kosa. Eleza dhana hii kama ilivyojitokeza katika
riwaya hii. (Al.20)
14.Tamthilia ya Kifo Kisimani haijapitwa na wakati. Jadili. (Al. 20)
15.Vita vya kikabila huchangia asilimia kubwa katika ukosefu wa
amani na kuleta ukimbizi Barani Afrika. Kwa kuirejelea hadithi fupi ya
Mkimbizi-John Habwe, fafanua shida zinazowakumba wakimbizi. (Al. 20)
16.Kwa kuirejelea tamthilia ya Kifo Kisimani-Kithaka wa Mberia,
eleza jinsi mwandishi anavyosawiri maudhui ya uzalendo. (Al.20
17.
Uovu wa uongozi katika nchi zinazokua umejikita barabara katika
tamthilia ya Kifo Kisimani-Kithaka wa Mberia. Thibitisha. (Al.20)
18.Eleza jinsi dhuluma dhidi ya haki za watoto inavyojitokeza kwa
kurejelea adithi fupi za Uteuzi wa Moyoni, Kachukua Hatua Nyingine,
Ngome ya Nafsi na Fumbo la Mwana. (Al.20)
19.Mwandishi ametumia mwanamke kama mhusika mojawapo wa kukuza azma
na maudhui yake katika riwaya ya Mwisho wa Kosa-Z. Burhani. Eleza nafasi
ya mwanamke katika riwaya hii. (Al. 20)
20.Mwandishi ametumia mbinu ya sadfa kama mojawapo ya kukuza azma na
maudhui yake katika riwaya ya Mwisho wa Kosa. Eleza mbinu hii kama
inavyosawirika riwayani. (Al. 20)
21.Ukinzano ni jambo la
kawaida katika jamii. Thibitisha ukirejelea riwaya ya Mwisho wa Kosa-
Z.
Burhani.
22.Kusameheana ndiyo dawa ya
waja. Tetea kauli hii ukiirejelea riwaya ya Mwisho wa
Kosa-
Z. Burhani.
23. Ni nini maana ya wimbo?
Taja mambo yanayotambulisha nyimbo. Eleza aina tofauti za nyimbo na
utaje umuhimu wake. Taja dhima ya nyimbo katika utambaji au katika
maigizo.
24. Eleza maana ya miviga,
mifano na dhamira yake.
25. Eleza makala makuu ya
Fasihi Simulizi. Tofautisha kati ya Fasihi Andishi na Fasihi
Simulizi.
26. Tofautisha kati ya
mighani na maghani. Taja sifa mbalimbali za mighani.
27. Maghani ni nini? Taja
aina mbili kuu za maghani na ueleze vijipengele vyake.
|