| |
|
Marudio Kamili ya Kiswahili KCSE
...Na David Ndegwa
Bei Ksh. 300/- |
 |
 |
Kitabu hiki kimebuniwa kuwasaidia wanafunzi wote katika shule za
sekondari pamoja na walimu ambao wanawatayarisha wanafunzi kwa
mtihani wa KCSE Kimekusanya mfululizo wa mifano ya maswali ambayo
mwanafunzi anaweza kuyapata katika mtihani wa KCSE. Maswali haya
yametungwa kwa ustadi na yamelenga nyanja muhimu katika silabasi
mpya ya somo la Kiswahili itakayotahiniwa kwa mara ya kwanza mwaka
wa 2006. Sehemu hizi ni: Matumizi ya Lugha, Mafumbo, Isimu Jamii na
Fasihi Simulizi. Mwandishi ametoa majibu kwa kila swali ili
mwanafunzi aweze kujitahini na kujipima mwenyewe bila kumtegemea
mwalimu.
|
MAELEZO ZAIDI...
Sehemu ya A ina maswali ya matumizi ya lugha pamoja na majibu.
Sehemu ya B ina maswali ya mafumbo pamoja na majibu, Sehmu ya C,
maswali ya Fasihi Simulizi pamoja na majibu na sehemu ya D, maswali
ya Isimu Jamii pamoja na majibu. |
| |
|
Nuru ya Isimu Jamii
... Na david Ndegwa
Bei Ksh.
300/- |
 |
Lengo la kukiandika kitabu hiki
ni kuwaelekeza wanafunzi katika shule za sekondari kwenye vipengele
vya msingi vya somo la Isimu Jamii. Ni dhahiri kwamba ufundishaji wa
somo hili bado ni mchanga mno na kwa hivyo inatarajiwa kuwa kitabu
hiki ni tunu kubwa kwa walimu na wanafunzi.
Kichocheo kikubwa cha matayarisho ya Nuru ya Isimu Jamii ni kujaza
pengo ambalo limekuwepo la somo hili. Walimu na wanafunzi
wamelalamika sana kwa ukosefu wa kitabu mwafaka cha marejeleo.
Mwandishi amekusudia kitabu hiki kiwe nuru katika eneo ambalo hadi
sasa limekuwa na giza totoro. Ametalii kwa undani vipengele vingi
muhimu vya Isimu Jamii pamoja na kuangazia mtalaa wa Isimu kwa jumla.
Natumai kwamba yaliyomo yatawazindua na kuwa hamasisha wasomaji wote
waanze kufanya utafiti zaidi na kukuza somo hili la Isimu Jamii.
Mwandishi amekusanya maswali mengi ya kufanyia mazoezi na
amependekeza majibu kwa baadhi ya maswali hayo ili kitabu kiweze
kuwa cha manufaa kamili kwa msomaji. |
| |
|
Iwapo unataka kuwasilisha vitabu vyako
kwetu au kujipatia nakala ya mojawapo ya vitabu hivi, tuandikie
barua ukitumia anwani
kiswahili@gskool.com |