MASHAIRI YETU  
l
 Mashairi
Yetu
Lala kwa Kadri
Asiliye Wapi?
Vijulanga Bandilikeni
Ulimi wanikanganya

 

 

Chumba cha Majadiliano>>>  Tuma Maswali/majibu>>>
 
Vijulanga Bandilikeni Na Allan Wadi
Nashika kuandika, bayana kuwaeleza,
Ukweli wa hakika, mbelenu wajitokeza,
Kwa kweli naudhika, kwa maovu mnayopoza,
Manani kawapenda, nanyi kajitia ambo.

Enyi vijana nasikitika, na hulka zenu za kuudhisha,
Mambo ya Mola mwakiuka, mkitafutana kama panza,
Hamjui mnakotoka, hamumu kawajaza,
Manani kawapenda, nanyi kajitia ambo.

Mmekuwa masika, yasiyojali Firauni wala Muza,
Mambo yote mmeyaruka, kwa ujanja wa ajuza,
Mkimwita Lusifa kaka, msikojua anakowaelekeza,
Manani kawapenda, nanyi kajitia ambo.

Nawasihi kutanzuka, na mambo ya tanza,
Na mwelewe fika, haya ninayowaeleza,
Mfuate mamlaka, na mtupilie mbali manza,
Manani kawapenda, nanyi kajitia ambo.

Nawarai muwe mbarika, na pia wabaraza,
Ya Ibilisi yakwajuka, kwa juhuda zenu za kuruza,
Hapo mtakuwa mmelimka, na hata kupendeza,
Manani kawapenda, nanyi kajitia ambo.

Omega nafika, baada ya kubonyeza,
Yanayohitajika kukoka, na pia ya Mungu kukoleza,
Nyoyo zenu zibadilika, na maovu kuyazinza,
Manani kawapenda, nanyi kajitia ambo.
 

 


Haki zote zimehifadhiwa. Kunakili Makala yoyote kutoka Kwenye Tovuti Hii Bila Idhini Iliyoandikwa na Wakurugenzi Hakuruhusiwi. Makala yote yanamilikiwa na Gskool.com punde tu yanapotumwa.
Tuma Mchango wako
au maswali kwa kiswahili@gskool.com.
Home 
Forums and Discussions  Legal  Contacts  Faqs

©Gskool Educational Site