|
Chumba cha Majadiliano>>>
Tuma Maswali/majibu>>>
UTANGULIZI
Ushairi ni matumizi ya lugha isiyo ya
kawaida katika kupitisha ujumbe fulani. Mashairi yanaweza kukaririwa au
kuimbwa kulingana na madhumuni na mbinu anyotaka kutumia manju. Katika
ushairi tunakutana na watu wawili ambao wana umuhimu mkubwa katika
kupitisha ujumbe kwa wanadamu kuhusu jambo fulani.
Ushairi hutumika kama mbinu muhimu ya
kupitisha ujumbe, uwe wa pongezi, maoni, kurekebisha, na kadhalika.
Katika ushairi, kunazo mbinu nyingi za uandishi wa mashairi na vivyo
vivyo kuna aina mbalimbali za mashairi.
Kunayo mashairi ya arudhi au ya kimapokeo.
Haya ni mashairi yanayofuata sheria za ushairi ambazo zinakubalika
katika utunzi wa mashairi.
Pia kunayo mashairi huru ambayo hayafuati
sheria zozote za ushairi. Mashairi haya huwa hayatumii mpangilio wowote
maalum. Kwa watunzi wa mashairi walibombea katika uwanda huu, mashairi
haya haykubaliki.
Tunazidi kukuandalia makala chungu nzima
katika ushairi. kuwa huru kuwasilisha mashairi yako kwetu na tutayaweka
katika tovuti yetu.
Soma Shairi Letu-Lala
kwa Kadri |