| |
    


|
4.0.0 KUANDIKA
4.1.0 Shabaha
Kufikia mwisho wa mafunzo ya Kiswahili
katika shule ya upili mwanafunzi aweze:
- kuandika hati nadhifu zinazosomeka;
- kuzingatia tahajia sahihi katika
maandishi;
- kuandika miundo sahihi ya sentensi;
- kuakifisha maandishi ipasavyo;
- kuandika maandishi yenye mtiririko wa
mawazo;
- kubuni na kuandika kwa kuzingatia
kanuni mbalimbali za utungaji;
- kuandika mikusanyo ya fasihi simulizi
ili kuihifadhi.
4.2.0 Yaliyomo
4.2.1 Uandishi wa kawaida:
Majibu ya
ufahamu, mukhtasari, imla na uchambuzi/uhakiki wa
maandishi
mbalimbali
4.2.2 Utungaji wa kiuamilifu:
Barua (kirafiki, rasmi, memo, simu, kwa
mhariri, meme -nukulishi, mdahilishi, ujumbe wa rununu/simu-tamba),
Hotuba, Ratiba k.m. tamasha za michezo ya kuigiza, Matangazo, Maagizo/maelezo,
Tahadhari (ilani, na onyo), Tawasifu, Shajara, Kumbukumbu, Mahojiano na
dayolojia, Insha za kitaaluma k.m. makala ya redio na runinga, Resipe,
Orodha ya mambo, Taarifa, Hojaji, Kujaza fomu, stakabadhi na orodha,
Risala
4.2.3 Uandishi wa Insha:
Methali,
Masimulizi, Mazungumzo, Mawazo, Maelezo, Mdokezo
4.2.4 Utungaji wa kisanii
a) Mashairi:i) Mashairi ya arudhi, ii)
Mashairi huru
b) Mikusanyo ya kazi za kisanii
c) Vitendawili, mafumbo na chemsha bongo
d) Vitanza ndimi
e) Michezo ya kuigiz f)
Tahakiki za kazi za kisanii.
4.2.5 Uakifishaji
- Kuakifisha maandishi ya aina
mbalimbali
- Usemi halisi
- Usemi wa taarifa.
4.2.6 Uundaji wa maneno
- Nomino kutokana na mzizi wa nomino
- Nomino kutokana na mzizi wa kitenzi
- Kitenzi kutokana na mzizi wa nomino
- Kivumishi kutokana na mzizi wa nomino
- Nomino kutokana na mzizi wa kivumishi
- Kivumishi kutokana na mzizi wa
kitenzi
- Kitenzi kutokana na mzizi wa kivumishi
4.2.7 Uundaji wa nomino
Nomino kutokana na vitenzi vya asili ya kigeni
Ukurasa wa
1
2
3
4 5 6
7 8
Chumba cha Majadiliano>>>
Tuma Maswali/majibu>>> |
|