Silabasi

   Silabasi ya Somo la Kiswahili (K.C.S.E  102)  
l
 


 

 

SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA
11. Sentensi ya Kiswahili

      a) Aina za:
        i) Virai: vihusishi, nomino, vivumishi, na vielezi.
        ii) Vishazi: huru na tegemezi

      b) Muundo wa sentensi
         i) Miundo ya kikundi/nomino (KN)
        ii) Miundo ya kikundi/tenzi (KT)
        iii) Yambwa/shamirisho (SH): kipozi, kitondo, ala/kitumizi
        iv) Chagizo (CH)

     c) Aina za sentensi: i) Sahili, Ambatano, Changamano

     d) Uchanganuzi/upambanuzi wa aina mbalimbali za sentensi kwa njia ya

    e) Jedwali,Mchoro wa matawi, Mstari

12. Uakifishaji:  Matumizi sahihi ya alama za kuakifisha:

         Nukta/kitone/kikomo (.),
         Mkato/kitone/kipumuo/kituo/koma (,),
         Nukta mkato/semi koloni (;),
         Nukta pacha/nukta mbili/koloni (:),
         Kiulizi/kiulizo (?),
         Alama hisi (!),
         Alama mtajo/za kunukuu/za usemi (" "),
         Mkwaju/mshazari (/),
         Kistari kifupi (-),
         Kistari kirefu ( - ),
         Mstari (_______),
         Ritifaa/kibainishi (‘),
         Mabano/vifungo/Parandesi ( ),
         Herufi kubwa (H) na herufi ndogo (h),
         Herufi nzito (Hh), Herufi mlazo/italiki (Hh),
         Nukta za dukuduku/mdokezo (…),
         Kinyota (*)

13. Uakifishaji:
Uakifishaji wa maandishi ya aina mbalimbali k. m. sentensi, aya, vifungu n.k. 14. Usemi halisi na usemi wa taarifa a) Usemi halisi b) Usemi wa taarifa 3.0.0 KUSOMA 3.1.0 Shabaha Kufikia mwisho wa mafunzo ya Kiswahili katika shule ya upili mwanafunzi aweze:

 •  kusoma kwa sauti na kuzingatia matamshi bora;
 •  kusoma kimya na kubainisha mawazo makuu pamoja na matumizi ya lugha;
 •  kuimarisha kusoma kwa kasi;
 • kufahamu na kujibu maswali kwa usahihi na kutekeleza ipasavyo;
 • kukuza uwezo wa kutumia maktaba;
 • kutumia kamusi ipasavyo;
 • kukuza dafina ya msamiati na muktadha na kaida za jamii;
 • kubainisha maadili na mafunzo yanayotokana na maandishi kwa Kiswahili;
 • kusoma kwa kina na kuchambua maandishi kwa Kiswahili;
 • kustawisha umilisi wa matumizi ya msamiati kutegemea muktadha na kaida za jamii;
 • kuelezea historia na chimbuko la Kiswahili na kuonea fahari kama lugha ya taifa letu;
 • kuzingatia maadili na mafunzo yanayojitokeza katika maandishi kwa Kiswahili;
 • kuelezea hali ya Kiswahili nchini Kenya baada ya uhuru na kuionea fahari kama lugha ya taifa na kimataifa;
 •  kufahamu, kujibu maswali kwa usahihi na ipasavyo.

Ukurasa wa 1  2  3 4 5 6 7 8
Chumba cha Majadiliano>>>  Tuma Maswali/majibu>>>

 


Haki zote zimehifadhiwa. Kunakili Makala yoyote kutoka Kwenye Tovuti Hii Bila Idhini Iliyoandikwa na Wakurugenzi Hakuruhusiwi. Makala yote yanamilikiwa na Gskool.com punde tu yanapotumwa.
Tuma Mchango wako
au maswali kwa kiswahili@gskool.com.
Home 
Forums and Discussions  Legal  Contacts  Faqs

©Gskool Educational Site