Silabasi

   Silabasi ya Somo la Kiswahili (K.C.S.E  102)  
l
 

 

 

 

 

 

 


 

 

2.1.0 SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA
2.1.1 Shabaha
Kufikia mwisho wa mafunzo ya kiswahili katika shule ya upili mwanafunzi aweze:

  1. kubainisha maana na dhima ya lugha;
  2. kueleza misingi ya uainishaji wa maneno ya Kiswahili;
  3. kukuza uwezo wa kutumia sauti, maneno ya Kiswahili sanifu katika mawasiliano ya kimazungumzo na kimaandishi;
  4. kutambua na kurekebisha makosa ya kisarufi na matumizi ya lugha/kimantiki;
  5. kukuza uwezo wa kutumia msamiati na istilahi;
  6. Kufafanua maana na aina za tungo;
  7. Kuchanganua sentensi na kufafanua maana, aina na vijenzi vya sentensi.

2.1.2 Yaliyomo
   1.  Lugha
        a) Maana na dhima ya lugha
        b) Sauti: Irabu/vokali, Konsonanti, Mpangilio wa sauti katika silabi na maneno
        c) Vipashio vya lugha: sauti-silabi-neno- sentensi

  2. Misingi ya maneno
        a) Mofimu:
           i) Maana na
          ii) Aina
              - Huru
              - Tegemezi

      b) Viambishi –
         i) maana na
         ii) aina
           - Awali
           - Tamati

  3. Aina za maneno na migawanyiko yake:
       Aina za maneno

      a) Nomino N - jumla/kawaida, pekee, dhania, kitenzi jina, jamii, na nomino za wingi.
      b) Vivumishi V – sifa, , vionyeshi, vimilikishi, viulizi, idadi, pekee, majina, unganifu,
           virejeshi, na visisitizi
     c) Vitenzi T - vitenzi halisi, vitenzi vikuu, visaidizi, vishirikishi vipungufu, vishirikishi vikamilifu, na vitenzi
        sambamba
    d) Viwakilishi N – vionyeshi, vimilikishi, viulizi, virejeshi, ‘A’ unganifu, sifa, nafsi, ngeli, pekee, idadi,
        visisitizi, na ‘O’ rejeshi
    e) Vielezi E - Vielezi vya:

          i) Namna/jinsi – vikariri, halisi, mfanano, hali, ala/vitumizi, na viigizi.
          ii) Wakati – viambishi na idadi/jumla
         iii) Idadi/Kiasi - idadi halisi na maneno kamili
         iv) Mahali – viambishi na maneno kamili

     f) Viunganishi U
     g) Vihusishi H
     h) Vihisishi

Ukurasa wa 1  2  3 4 5 6 7 8
Chumba cha Majadiliano>>>  Tuma Maswali/majibu>>>

 


Haki zote zimehifadhiwa. Kunakili Makala yoyote kutoka Kwenye Tovuti Hii Bila Idhini Iliyoandikwa na Wakurugenzi Hakuruhusiwi. Makala yote yanamilikiwa na Gskool.com punde tu yanapotumwa.
Tuma Mchango wako
au maswali kwa kiswahili@gskool.com.
Home 
Forums and Discussions  Legal  Contacts  Faqs

©Gskool Educational Site