Silabasi

   Silabasi ya Somo la Kiswahili (K.C.S.E  102)  
l
 


 

 

1.1.0 KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
1.1.1 Shabaha
      
Kufikia mwisho wa mafunzo ya Kiswahili katika shule ya upili, mwanafunzi aweze:
 1. a) kuzingatia, kuimarisha na kuendeleza umilisi na uzoefu wa matamshi bora katika lugha ya Kiswahili;
 2. b) kutambua na kurekebisha athari zitokanazo na lugha za mama na lugha nyinginezo;
 3. c) kustawisha mawasiliano yafaayo kulingana na kaida za jamii kutegemea mahusiano, mada na mahitaji ya sajili;
 4. d) kusikiliza, kufahamu na kutekeleza ipasavyo;
 5. e) kubuni na kujieleza kikamilifu na kimantiki;
 6. f) kukuza uwezo wa kukusanya na kuhifadhi kazi za fasihi simulizi
 7. g) kukuza utendaji wa kisanii;
 8. h) kukuza kiwango cha msamiati kwa ajili ya mawasiliano mbalimbali;
 9. i) kuzungumza lugha ya Kiswahili kwa ufasaha na kuionea fahari;
 10. j) kuzingatia na kuhakiki na kuchanganua kazi mbalimbali za fasihi;
 11. k) kueleza historia na maendeleo ya Kiswahili na kuionea fahari kama lugha ya taifa letu;
 12. l) kuzingatia mafunzo na maadili yanayojitokeza katika kazi mbalimbali kwa Kiswahili;
 13. m) kueleza nafasi ya Kiswahili nchini kama lugha ya taifa na kimataifa.

Ukurasa wa 1  2  3 4 5 6 7 8
Chumba cha Majadiliano>>>  Tuma Maswali/majibu>>>

 


Haki zote zimehifadhiwa. Kunakili Makala yoyote kutoka Kwenye Tovuti Hii Bila Idhini Iliyoandikwa na Wakurugenzi Hakuruhusiwi. Makala yote yanamilikiwa na Gskool.com punde tu yanapotumwa.
Tuma Mchango wako
au maswali kwa kiswahili@gskool.com.
Home 
Forums and Discussions  Legal  Contacts  Faqs

©Gskool Educational Site