| |
    


|
MADHUMUNI YA UJUMLA
Kuendeleza mafunzo ya Kiswahili yaliyoshughulikiwa katika shule
za msingi.
Kumpa mwanafunzi uwezo wa kudumu wa kusikiliza, kuzungumza,
kusoma na kuandika ipasavyo kwa lugha ya Kiswahili.
Kumwezesha kubuni, kuchambua na kujieleza wazi kimantiki.
Kutumia Kiswahili katika mawasiliano na shughuli za kila siku.
Kutambua, kudadisi, kuthamini na kustawisha aina na tanzu
mbalimbali za lugha na fasihi kwa Kiswahili.
Kujifunza na kuthamini fani mbalimbali za tamaduni kwa kutumia
Kiswahili.
Kuwa na utambuzi kwa mambo yanayohusu na yanayoiathiri jamii
k.m. ukimwi, maendeleo ya kiteknolojia, usawa wa kijinsia n.k.
Kuhifadhi mazingira kwa ajili ya kudumisha uhai na kujitimizia
mahitaji ya kila siku na ya maisha ya baadaye.
Kufurahia kujisomea na kujiendeleza mwenyewe kadiri ya uwezo
wake.
Kuthamini, kufurahia na kujivunia Kiswahili kama lugha ya
taifa na kimataifa.
Ukurasa wa
1
2
3
4 5 6
7 8
Chumba cha Majadiliano>>>
Tuma Maswali/majibu>>>
|
|