MASHAIRI YETU  
l
 Mashairi Yetu
Lala kwa Kadri
Asiliye Wapi?
Vijulanga Bandilikeni
Ulimi wanikanganya

 

 

Chumba cha Majadiliano>>>  Tuma Maswali/majibu>>>
 
Asiliye Wapi?  Na Alfonce Nzioka
Mbele yenu nasimama, bila kusitasita
Kwa bayana ninasema, damu kinipwitapwita
Kwa bashasha naungama, swali lililotata
Wapi asili ya kiswahili?

Asili yake Afrika, mahuluki ataa’za
Labda chanzoke Ika, mwingine atajiwaza
Lakini kusema fika, asiliye yaniduwaza
Wapi asili ya kiswahili?

Jawabu fika hakuna, kwa alaa kulihali
Mathalani ninaguna, nakeketwa na jiswali
Siwezi kamwe kukana, sitaacha kusaili
Wapi asili ya kiswahili?

Nibandike jina juha, au la Bozibozi
Sina budi kunadi ha! Kweli wewe wamaizi?
Katu sichoki kuhaha, nauliza kwa uwazi
Wapi asili ya Kiswahili?
 

 


Haki zote zimehifadhiwa. Kunakili Makala yoyote kutoka Kwenye Tovuti Hii Bila Idhini Iliyoandikwa na Wakurugenzi Hakuruhusiwi. Makala yote yanamilikiwa na Gskool.com punde tu yanapotumwa.
Tuma Mchango wako
au maswali kwa kiswahili@gskool.com.
Home 
Forums and Discussions  Legal  Contacts  Faqs

©Gskool Educational Site