SEMI ZA JOZI  
l
 


>>
Isimu Jamii
>>Semi za Jozi
 
 

 

Chumba cha Majadiliano>>>  Tuma Maswali/majibu>>>

Haya ni maneno mawili ambayo huwa yakifuatana ili kutimiza jozi. Mfuatano huu hutilia mkazo na huweza kuleta ubainisho zaidi na mahusiano au tofauti kati ya vitu viwili vinavyozungumziwa mifano ni haya:

• Alfa na omega:   mwanzo na mwisho
• Asili na jadi:   yasiyoweza kusahaulika.
• Baba na mama :   Kuwa pamoja kama wazazi.
• Balaa na beluwa:   Matatizo na makosa mengi.
• Daima na dahari :   Siku nyingi
• Dhiki na faraja:   Hali ya utulivu na shida
• Ficha na fichua:   kusitiri na kuonyesha
• Hali na mali :   Tayari kujitolea kwa vyote
• Hapa na pale :   Sio mbali sana
• Inda na inadi :   Ujeuri na maudhi
• Jahazi na tanga :   zinazotegemeana
• Jembe na mpini :   Kushika vizuri ili kutimiza jambo.
• Jicho na kidole :   Uadui wa hali ya juu
• Kalamu na karatasi :   Jinsi zinavyosaidiana kutimiza barua.
• Kiguu na njia :   Kutopumzika saa zote mbioni.
• Kijibwa na bwanshira :  kufuatana saa zote.
• Kinu na mchi :   Kusaidiana
• Kondoo na mbwa :  uadui wa hali ya juu.
• Kurwa na doto :   Wapenzi wasioachana
• Sahani na kawa:   vilivyolingana
• Sakafu na dari :   zinavyoelekeana saa zote.
• Shibe na njaa :   hali zote mbili; furaha na dhiki
• Siri na dhahiri:   Kuficha na iliyowazi kujulikana
• Udi na uvumba:   kwa hali zote

Waweza kutuma insha yako kwetu na waweza kuwa mshindi wa tuzo letu
Endelea kusoma makala zaidi upate umaarufu.

 


Haki zote zimehifadhiwa. Kunakili Makala yoyote kutoka Kwenye Tovuti Hii Bila Idhini Iliyoandikwa na Wakurugenzi Hakuruhusiwi. Makala yote yanamilikiwa na Gskool.com punde tu yanapotumwa.
Tuma Mchango wako
au maswali kwa kiswahili@gskool.com.
Home 
Forums and Discussions  Legal  Contacts  Faqs

©Gskool Educational Site