Uandishi wa Insha

Insha ni utungo ambao kwa mara nyingi huwa ni maoni ya mwandishi. Kwa mara nyingi, insha huandikwa kwa ajili ya mitihani lakini kumbuka kwamba insha inaweza kuandikwa kama kumbukumbu ya matukio fulani mbila madhumuni ya kutahiniwa.

Kwa kufuatia mfumo wa sasa wa elimu Nchini Kenya, kuna insha za aina mbalimbali ambazo mwanafunzi anaweza kutahiniwa kama vile

  • Insha za Kubuni
  • Insha za Barua
  • Insha za Hotuba
  • Insha za “Kuendeleza Kifungu Fulani”
  • Isha za kumbukumbu
  • n.k

Katika uandishiwa insha mwanafunzi anastahili kuzingatia mambo mbali mbali ambayo yanaweza kufanikisha uandishi wainsha yake.

Kwanza kabisa tahajia lazima iwe ya kuvutia na kupendeza. Hili huifanya insha kuweza kusomeka kwa urahisi jambo ambalo huwafurahisha watahini wengi.

Pili mwanafunzi anastahili kuzingatia maendelezo na kuhakikisha kwamba insha yake haina makosa yoyote ya maendelezo. Isisahaulike kwamba kila kosa la maendelezo hutozwa alama, hadi alama zifikapo tano.

Mfululizo wa mawazo pia ni jambo la kuzingatia vilevile. Kusoma inha isiyo na mfululizo mwema ni kama kuendesha gari katika baraste yenye mawe na visiki. Dereva hawezi kufurahia kuendesha gari katika baraste kama hiyo na vivyo hivyo mtahini hawezi kufurahia kusoma insha kama hiyo.

Isitoshe, mwanafunzi anastahili kuandika insha akifuata mfululizo unaokubalika katika uandishi. Kwa mfano huwezi kuandika barua rasmi ukitumia aya kama ilivyokuwa hapo awali.

Haya na mengine mengi yanastahili kuzingatiwa ili kuhakikisha kwamba insha yenyewe ina ladha na bila shaka huwezi kukosa kupata alama za juu.

You can leave a response, or trackback from your own site.

Andika Maoni/Jibu