3. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA

4. Ngeli za nomino –
A – WA, U – I, U – YA, YA – YA, LI – YA, KI – VI, I – ZI, I – I, U – ZI, U – U, KU -, PA-KU-MU.
5. Umoja na wingi
Ngeli za nomino k.m. A-WA , U-I, LI-YA n.k. na upatanisho wa kisarufi kwa mintaarafu ya viambishi:
a) Awali vya vitenzi
b) Vya vivumishi vya sifa
c) Vya vivumishi vya pekee – enye, -enyewe, -ingine, -ote, -o-ote, -ingineo

6. Misingi ya maneno
a) Mofimu
i) Maana na
ii) Aina     – Huru ,    – Tegemezi
b) Viambishi –
i) Maana na
ii) Aina     – Awali,   – Tamati

7. Matumizi ya maneno na viambishi maalumu
a) Viambishi: -ku-, -ndi-, -ji-
b) Maneno: Jinsi, Namna, Ila, Japo, Ijapokuwa, Ingawa, Ingawaje, Ikiwa, Wala, Walakini, Kwa, Labda, Na

8. Nyakati na hali
a) Nyakati: LI, NA, TA
b) Hali: ME, HU, NGE, NGELI, NGALI, A, KA, KI, KU
c) Hali ya kuamuru
d) Ukanushaji kutegemea nafsi na: i) Nyakati, ii) Hali

i) Nyakati
– Uliopita -LI-
– Uliopo -NA, – Ujao – TA-
ii) Hali – Hali timilifu -ME- – Hali ya mazoea -HU-
iii) Ukanushaji kutegemea nafsi na: – Nyakati – LI-, -NA-, -TA- – Hali -ME-HU-

9. Mnyambuliko wa vitenzi
a) Kauli za vitenzi – Kutendwa, Kutendewa, Kutendeka, Kutendana, Kutendeana, Kutendeshwa,
Kutendeshana, Kutendeshea, Kutenda, Kutendesha

b) Mnyambuliko wa vitenzi vya: Asili ya kigeni, , Silabi moja, Asili ya kibantu,

c) Kauli za vitenzi vya kibantu: Kutendeshewa, Kutendesheana, Kutendesheka, Kutendama,
Kutendata, Kutendua, Kutenduka

d) Mnyambuliko wa vitenzi vya silabi moja katika kauli mbalimbali:
ja, nywa, nya, pa, fa, la, cha, pwa, chwa, wa

e) Mnyambuliko wa vitenzi vyenye asili ya kigeni k.m. samehe, ghairi, tubu, n.k. katika kauli mbalimbali.

10. Sentensi ya Kiswahili
a) Maana ya sentensi
b) Mpangilio na uhusiano wa maneno kimantiki katika sentensi ya Kiswahili.

11. Sentensi ya Kiswahili
a) Aina za:
i) Virai: vihusishi, nomino, vivumishi, na vielezi.
ii) Vishazi: huru na tegemezi

b) Muundo wa sentensi
i) Miundo ya kikundi/nomino (KN)
ii) Miundo ya kikundi/tenzi (KT)
iii) Yambwa/shamirisho (SH): kipozi, kitondo, ala/kitumizi
iv) Chagizo (CH)

c) Aina za sentensi: i) Sahili, Ambatano, Changamano

d) Uchanganuzi/upambanuzi wa aina mbalimbali za sentensi kwa njia ya

e) Jedwali,Mchoro wa matawi, Mstari

12. Uakifishaji:  Matumizi sahihi ya alama za kuakifisha:

Nukta/kitone/kikomo (.),
Mkato/kitone/kipumuo/kituo/koma (,),
Nukta mkato/semi koloni (;),
Nukta pacha/nukta mbili/koloni (:),
Kiulizi/kiulizo (?),
Alama hisi (!),
Alama mtajo/za kunukuu/za usemi (” “),
Mkwaju/mshazari (/),
Kistari kifupi (-),
Kistari kirefu ( – ),
Mstari (_______),
Ritifaa/kibainishi (‘),
Mabano/vifungo/Parandesi ( ),
Herufi kubwa (H) na herufi ndogo (h),
Herufi nzito (Hh), Herufi mlazo/italiki (Hh),
Nukta za dukuduku/mdokezo (…),
Kinyota (*)

13. Uakifishaji:
Uakifishaji wa maandishi ya aina mbalimbali k. m. sentensi, aya, vifungu n.k. 14. Usemi halisi na usemi wa taarifa a) Usemi halisi b) Usemi wa taarifa 3.0.0 KUSOMA 3.1.0 Shabaha Kufikia mwisho wa mafunzo ya Kiswahili katika shule ya upili mwanafunzi aweze:

 • kusoma kwa sauti na kuzingatia matamshi bora;
 • kusoma kimya na kubainisha mawazo makuu pamoja na matumizi ya lugha;
 • kuimarisha kusoma kwa kasi;
 • kufahamu na kujibu maswali kwa usahihi na kutekeleza ipasavyo;
 • kukuza uwezo wa kutumia maktaba;
 • kutumia kamusi ipasavyo;
 • kukuza dafina ya msamiati na muktadha na kaida za jamii;
 • kubainisha maadili na mafunzo yanayotokana na maandishi kwa Kiswahili;
 • kusoma kwa kina na kuchambua maandishi kwa Kiswahili;
 • kustawisha umilisi wa matumizi ya msamiati kutegemea muktadha na kaida za jamii;
 • kuelezea historia na chimbuko la Kiswahili na kuonea fahari kama lugha ya taifa letu;
 • kuzingatia maadili na mafunzo yanayojitokeza katika maandishi kwa Kiswahili;
 • kuelezea hali ya Kiswahili nchini Kenya baada ya uhuru na kuionea fahari kama lugha ya taifa na kimataifa;
 • kufahamu, kujibu maswali kwa usahihi na ipasavyo.
  You can leave a response, or trackback from your own site.

  Andika Maoni/Jibu