Maswali ya hafla ya Mdahalo wazi, Shule ya Wavulana ya Starehe

KENYA HIGH SCHOOL

Wanafunzi wako watashughulikia maswali yafuatayo:

 1. 1. Eleza maana ya sentensi: “Ningalikuwa na pesa ningalinunua nyumba ningalistarehe”
 2. 2. Badilisha sentensi ifuatayo ili iwe katika hali ya kuamuru: Baba ingia ndani.
 3. 3. Ainisha viambishi katika neno: kujidhiki

NGARA GIRLS

Wanafunzi wako watashughulikia  maswali yafuatayo.

 1. 1. Tambua na ueleze aina za vivumishi katika sentensi zifuatazo.
  i) Mtoto mwenyewe alienda shambani.
  ii) Kazi yetu haihitajiki shuleni.
 2. 2. Tunga sentensi moja moja kuonyesha tofauti kati ya vitate vifuatavyo
  i) Karama
  ii) Gharama

MT. LAVENA

Wanafunzi wako watashughulikia maswali yafuatayo

TAMTHILIA

KITHAKA WA MBERIA: KIFO KISIMANI.

1             “Huu utakuwa mwanzo wa mwisho”

(a)         Eleza muktadha wa dondoo hili

(b)        Fafanua sifa na umuhimu wa anayeambiwa haya.

(c)        Dhihirisha vile usemi huu, “Mwanzo wa mwisho” ulivyotimia.

ST. GEORGES,

Wanafunzi wako watashughulikia maswali yafuatayo.

a) Ni nini maana ya maghani?

b)Taja na ueleze aina za maghani.

c)Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza sifa kuu za kimtindo zinazopatikana katika methali.

COMPUERA GIRLS

1.  Taja mbinu za lugha zilizotumiwa katika sentensi zifuatazo
i) Pema usijapo pema ukipema si pema tena
ii) Kaka yangu ni mrefu ja twiga

2.  Taja matumizi matatu ya neno ‘vile’

3. Tambua shamirisho kipozi katika sentensi ifuatayo.
Mama alinunua kitabu leo kabla hajasafiri

KAROTI GIRLS

(a)    Tofautisha dhana zifuatazo za fasihi simulizi.

(i) Ngomezi na Ngonjera

(ii) Wawe na Kimai

(b)   Taja na ueleze vizingiti vinne vya matumizi ya ngomezi siku hizi

(c)   Eleza muundo wa nyimbo kwa kutoa hoja nne toshelezi.

MACHAKOS BOYS SCHOOL

Wanafunzi wako watashughulikia maswali yafuatayo:

TAMTHILIA, KIFO KISIMANI

Kwa kutoa hoja kumi toshelezi, jadili jinsi uongozi mbaya unavyodhihirika katika Kifo Kisimani.

NAIVASHA GIRLS,

Wanafunzi wako watashughulikia maswali yafuatayo

a)     Taja mambo yanayopambanua muundo wa nyimbo katika jamii za kiafrika

b)     Ingawa nyimbo ni nzuri zina ubaya wake. Fafanua huku ukitoa mifano.

c)     Visasili vina umuhimu gani katika jamii.

d)       i)   Eleza maana ya maghani.

ii)  Taja aina mbili kuu za maghani.

AKIBA SCHOOL

Wanafunzi wako watashughulikia maswali yafuatayo: MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE

“Haiwezekani! Nitakwendaje Waziri mzima! Aibu!

Nitaonana na balozi wa nyumba kumi!”

a)         Eleza muktadha wa maneno haya ukirejelea hadithi ya Mayai waziri Wa Maradhi.

b)          Jadili maudhui ya uongozi mbaya kwa kutoa mifano yoyote sita.

c)         Neno kumi limetajwa kurejelea mambo kadhaa katika hadithi. Taja yoyote matano.

d)          Eleza sifa mbili za mzungumzaji katika dondoo.

SUNSHINE

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo: HADITHI FUPI

Hadithi za Msamaria Mwema na Kachukua Hatua Nyingine zinatuchorea picha ya jamii zenye uozo uliokithiri.Kwa kutoa mifano yoyote MITANO kwa kila hadithi, thibitisha ukweli wa kauli hii.

ALLIANCE GIRLS

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo: HADITHI FUPI

‘Na watakaompa yeye wamekosa kazi! Hebu yeye aweza kufanyani? Wanaume hawakuweza kufanya lolote aweza yeye?

a)         Eleza muktadha wa dondoo hili.

b)         Fafanua matokeo ya suala linalozungumziwa.

c)         Kwa kurejelea hadithi nzima, fafanua matatizo yanayomkumba mzungumziwa.

MANGU HIGH

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo: TAMTHILIA

(a)      Kwa kutoa hoja kumi, onyesha jinsi wahusika mbalimbali wanadhihirisha uzalendo chanya

katika tamthilia ya Kifo Kisimani.

(b)      Jadili matumizi matano ya mbinu ya Sadfa katika tamthilia ya Kifo Kisimani.

LORETO CONVENT LIMURU,

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo: RIWAYA (UTENGANO, S.A MOHAMMED)

Tazama, tazama watu walianza kuonyeshana, tazama ….. yule anakwenda wapi? Ana wazimu nini! Kuna nini?

(a)Eleza muktadha wa dondoo.

(b)Kwa kuitolea mfano, tambua mbinu ya lugha iliyotumika katika dondoo.                     

(c)Toa mifano yoyote saba iliyofafanuliwa inayoonyesha vile ambavyo maisha ya mrejelewa yalivyobadilika.                                                                                                                           

RIARA GIRLS SECONDARY SCHOOLS,

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

Hadithi ya ‘Mayai Waziri wa Maradhi’ inadhihirisha matatizo yanayozikumba nchi huru katika bara la  Afrika. Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano mwafaka katika hadithi.

NEMBU GIRLS

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

Tofautisha dhana zifuatazo za fasihi simulizi.                                                                               

(a) (i) Ngomezi na Ngonjera       (ii) Wawe na Kimai

(b) Taja na ueleze vizingiti vinne vya matumizi ya ngomezi siku hizi.                               

(c) Eleza muundo wa nyimbo kwa kutoa hoja nne toshelezi.

MARY HILL  GIRLS

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

(a) Eleza kwa kutolea mfano maana ya sauti ghuna.

(b) Kwa kutolea mifano, eleza maana ya
i)    kiimbo.   ii)           Mofimu huru         iii)           silabi mwambatano

AGA KHAN HIGH SCHOOL

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo: TAMTHILIA

“Bila shaka kuna shida. Kusingelikuwa na shida Mtemi Bokono angelikuwa anahutubia watu wake …….”

(i) Eleza muktadha wa dondoo hili.

(ii) Taja na ueleze mbinu ya lugha iliyotumika katika dondoo.                          

(iii) Eleza sifa zozote nane za msemaji.                                                                    

PANGANI GIRLS

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo; TAMTHILIA

Onyesha na kueleza kwa tafsiri mifano mitatu ya mbinu ya ndoto kulingana na ilivyotumika  katika Kifo Kisimani.

MOI FORCES ACADEMY

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo: TAMTHILIA

A:          Mtemi ataingia hivi punde. Na anatarajia kusikia habari nzuri ….

B:           Mtemi anataka kumsamehe kwa masharti gani?

a)         Eleza muktadha wa maneno haya.

b)         Mtemi anatarajia kusikia habari gani nzuri.

c)         Taja masharti ambayo yanarejelewa hapa.

d)         Jumuiya ya Butangi ililemewa na ufisadi. Eleza.

KAHUHIA SECONDARY SCHOOL

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo: FASIHI SIMULIZI

a) Eleza maana ya MIVIGA.

i)Taja sifa zozote nne za miviga.

ii)Taja umuhimu wa NYISO katika Fasihi Simulizi.

b) Eleza sifa zozote tatu za nyimbo zifuatazo.

i)           Bembezi    ii)          Mbolezi

PARKLANDS ARYA GIRLS HIGH SCHOOL

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

RIWAYA: UTENGANO

Kwa kutolea mifano mwafaka, jadili kauli kuwa Utengano ni riwaya tatizo.

EMBAKASI GIRLS,

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

Tumia viunganishi vingine badala ya hivi vilivyotumiwa.                                                                                            Anayetafuta hachoki hata akichoka keshapata.

Ngojeeni hadi washiriki wote wafike.

Tunga sentensi ukitumia kihusishi cha kuonyeshea.

i)           Mahali/ujirani

ii)           Kiwango

iii)           Kulinganisha

MT.KENYA ACADEMY SENIOR SCHOOL

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo: RIWAYA YA UTENGANO

“Mkubwa kabisa ni mwanchi. Umma ndio mkubwa kabisa na umma umeshautenda vya kutosha wewe …..”

a)         Eleza muktadha wa dondoo hili.

b)         Onyesha vile mzungumziwa alivyoutendea umma mabaya.

c)          Fafanua sifa zozote nne za anayezungumza.

BURUBURU GIRLS

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo: FASIHI SIMULIZI

Tofautisha dhana zifuatazo za fasihi simulizi.

(a) Taja na ueleze vizingiti vinne vya matumizi ya ngomezi siku hizi.                               

(b) Eleza muundo wa nyimbo kwa kutoa hoja nne toshelezi.

BRIGHTSTONE ACADEMY

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo: MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE.

Mayai Waziri Wa Maradhi.

‘Mimi nashughulika na wanyama wa porini, mambo yanayohusu binadamu mimi simo.’

a)         Eleza muktadha wa maneno haya.

b)         Onyesha jinsi mzungumzaji na wenzake wasivyowajali wananchi wanaowahudumia.

MOI GIRLS,

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE:

PWAGUZI

Pwagu hupata pwaguzi. Thibitisha ukweli wa kauli hii.

NGIRIAMBU GIRLS

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo.

FASIHI SIMULIZI.

a) Fafanua sifa nne za Ushairi Simulizi.

b) Eleza hasara mbili za majigambo.

c) Eleza umuhimu wa fomula ya ufunguzi katika ngano.

d) Itaje sifa kuu ya hurafa. Je, ni kwa nini sifa hiyo hutumiwa.

STAREHE GIRLS,

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

a) Jadili kwa kina matatizo matatu ambayo huenda yakaikabili Fasihi Simulizi katika jamii ya kesho kisha utoe mapendekezo ya jinsi ya kukabiliana na hali hii.

b) Fafanua sifa nne za Ushairi Simulizi.

c) Eleza hasara mbili za majigambo.

HURUMA GIRLS

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo: FASIHI SIMULIZI

a) Taja mambo yanayopambanua muundo wa nyimbo katika jamii za kiafrika.

b) Ingawa nyimbo ni nzuri zina ubaya wake. Fafanua huku ukitoa mifano.

BISHOP GATIMU

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo: FASIHI SIMULIZI

i ) Visasili vina umuhimu gani katika jamii.

ii) Eleza maana ya maghani.

iii) Taja aina mbili kuu za maghani.

iv) Eleza vipera vitatu vikuu vya maghani ya kawaida.

KABARE GIRLS

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo: LUGHA

a) i) Taja irabu mbili zinazotamkwa wakati mdomo umeviringwa.  ii) Taja irabu mbili zinazotamkwa katika sehemu ya mbele ya ulimi.

b)         Bainisha mzizi na viambishi tamati katika vitenzi vifuatavyo.   i) awaibiaye    ii)       alikeni

c)         Taja ngeli za majina yafuatayo.

i)           Mawaidha

ii)           Hatia

KYENI GIRLS

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

a) Eleza matumizi ya ni. i) Pesa zimo mfukoni.   ii) Moja na moja ni mbili.

b) Bainisha aina za virai katika sentensi hizi.

i)       Wazee na vijana walikuwa mkutanoni.

ii)       Mwanafunzi stadi alifuzu mtihani.

c) Bainisha matumizi ya Ji katika maneno yafuatayo.   i)              utajiumiza   ii)       ufundishaji

GOOD SHEPHERD GIRLS

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo.

a) Onyesha aina za shamirisho katika sentensi zifuatazo.

i)           Mzalendo amemwandikia mhariri barua.

ii)           Ali atatembea kwa miguu.

b) Bainisha vielezi katika sentensi hizi.

i)           Sudiata alimpenda mwanawe mno.

ii)           Tumeingia awamu ya pili.

STATE HOUSE GIRLS

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

Andika vitenzi vifuatavyo kulingana na maagizo kwenye mabano.

i)           Kokoa (kutendata)

ii)           Ficha (kutendama)

Bainisha aina za vitenzi katika sentensi hizi.

i)             Omari alikuwa daktari.

ii)           Jesse ni mwaminifu mno.

MAKUENI GIRLS

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo.

Tunga sentensi sahihi ukitumia viunganishi.

i)          Ila     ii) Licha ya

Andika sentensi kwa umoja.

i)           Walituibia nyimbo ndefu.

ii)           Theluji ya milima ya Afrika Mashariki imeanza kupungua.

Unda nomino nne kutokana na kitenzi kimbia.

PRECIOUS BLOOD KILUNGU

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

a) Andika katika usemi wa taarifa.

“Atakuarifu akimwona,” Vumilia alisema.

b) Eleza matumizi ya ni.

i)          Someni kwa bidii.     ii)        Pana wageni mlangoni nenda kawafungulie.

c) Eleza maana ya vitate hivi:

i)           Uga    ii) Unga

OFAFA JERICHO SECONDARY SCHOOL

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

S.A Mohammed: Utengano

Kwa kurejelea riwaya ya Utengano, fafanua maudhui yafuatayo.

-Utengano

-Nafasi ya mwanamke katika jamii

-Kisasi

-Uasi

OUR LADY OF MERCY SECONDARY SCHOOL

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

MAYAI WAZIRI WA MARADHI NA HADITHI NYINGINE – K.W. Wamitila

Mwanamume amechorwa vipi katika hadithi zifuatazo?

(a)Ngome ya Nafsi

(b)Kuchukua Hatua Nyingine

(c)Uteuzi wa Moyoni

LIMURU GIRLS

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

S.A MOHAMED: Utengano.

“Mbio za sakafuni huishia ukingoni”

Thibitisha ukweli wa methali hii ukirejelea wahusika tofauti katika riwaya ya Utengano.

LENANA SECONDARY SCHOOL

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

Eleza uozo wa jamii unavyojitokeza katika hadithi hizi.

a)Mayai waziri wa maradhi

b)Msamaria mwema

MAKUENI BOYS

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo: UTENGANO

Dhihirisha matumizi ya mbinu zifuatazo katika riwaya ya utengano:

i)Taharuki

(ii)Kisengere nyuma

(iii)Kinaya

NILE ROAD SECONDARY SCHOOL

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo]

a. Eleza maana ya kitendawili.

b. Taja sifa sita za vitendawili.

c. Eleza umuhimu wa vitendawili.

KERUGOYA GIRLS

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

Eleza sifa tano za nyimbo

Taja na ueleze aina zozote tano za nyimbo.

ST. TERESA’S GIRLS,

Wanafunzi wako watashughulikia swali lifuatalo

Popoo mbili zavuka mto

Tambulisha kipera kilichotajwa

Taja sifa zozote nne za kipera hiki

Taja mbinu zozote mbili zilizotumika katika kipera hicho.

Eleza dhima ya kipera hiki katika jamii.

You can leave a response, or trackback from your own site.

Andika Maoni/Jibu