4.0.0 KUANDIKA

4.1.0 Shabaha

Kufikia mwisho wa mafunzo ya Kiswahili katika shule ya upili mwanafunzi aweze:

 • kuandika hati nadhifu zinazosomeka;
 • kuzingatia tahajia sahihi katika maandishi;
 • kuandika miundo sahihi ya sentensi;
 • kuakifisha maandishi ipasavyo;
 • kuandika maandishi yenye mtiririko wa mawazo;
 • kubuni na kuandika kwa kuzingatia kanuni mbalimbali za utungaji;
 • kuandika mikusanyo ya fasihi simulizi ili kuihifadhi.

4.2.0 Yaliyomo
4.2.1 Uandishi wa kawaida:
Majibu ya ufahamu, mukhtasari, imla na uchambuzi/uhakiki wa
maandishi mbalimbali

4.2.2 Utungaji wa kiuamilifu:
Barua (kirafiki, rasmi, memo, simu, kwa mhariri, meme -nukulishi, mdahilishi, ujumbe wa rununu/simu-tamba), Hotuba, Ratiba k.m. tamasha za michezo ya kuigiza, Matangazo, Maagizo/maelezo, Tahadhari (ilani, na onyo), Tawasifu, Shajara, Kumbukumbu, Mahojiano na dayolojia, Insha za kitaaluma k.m. makala ya redio na runinga, Resipe, Orodha ya mambo, Taarifa, Hojaji, Kujaza fomu, stakabadhi na orodha, Risala

4.2.3 Uandishi wa Insha:
Methali, Masimulizi, Mazungumzo, Mawazo, Maelezo, Mdokezo

4.2.4 Utungaji wa kisanii
a) Mashairi:i) Mashairi ya arudhi, ii) Mashairi huru
b) Mikusanyo ya kazi za kisanii
c) Vitendawili, mafumbo na chemsha bongo
d) Vitanza ndimi
e) Michezo ya kuigiz f) Tahakiki za kazi za kisanii.

4.2.5 Uakifishaji

 • Kuakifisha maandishi ya aina mbalimbali
 • Usemi halisi
 • Usemi wa taarifa.

4.2.6 Uundaji wa maneno

 • Nomino kutokana na mzizi wa nomino
 • Nomino kutokana na mzizi wa kitenzi
 • Kitenzi kutokana na mzizi wa nomino
 • Kivumishi kutokana na mzizi wa nomino
 • Nomino kutokana na mzizi wa kivumishi
 • Kivumishi kutokana na mzizi wa kitenzi
 • Kitenzi kutokana na mzizi wa kivumishi

4.2.7 Uundaji wa nomino
Nomino kutokana na vitenzi vya asili ya kigeni

You can leave a response, or trackback from your own site.

Andika Maoni/Jibu