| |
    
>>Kifo
Kisimani
>>Mwisho wa Kosa
>>Mayai Waziri...
>>Fasihi Simulizi
>>Maswali Ya Ziada


|
Chumba cha Majadiliano>>>
Tuma Maswali/majibu>>>
NGANO:
Ngano ni hadithi ambazo hurithi kutoka kizazi kimoja hadi kingine
Sifa za Ngano:
i) Huwa na mianzio maalum k.m. Paukwa! Pakawa!
ii) Urudiaji wa maneno au matukio ili kusisitiza maudhui fulani.
iii) Matumizi ya nyimbo ili:
- kupunguza ukinaifu
- kubadilisha mtindo
- kuishirikisha hadhira
- kusisitiza ujumbe au maudhui
- kutumbuiza
iv) Mtuo wa kidrama ili kusisitiza ujumbe na kuongeza taharuki.
v) Matumizi ya tanakali sauti- kuongeza utamu na kuipa hadhira picha
kamili.
vi) Hutumia ishara-mwili ili kuonyesha picha na kuendeleza uelewaji.
vii) Mbinu ya ufaraguzi-kuigiza maneno, methali, misemo.
viii) Maswali ya balagha- kusisitiza ujumbe na kushirikisha hadhira.
ix) Miishio maalum- kutaja maadili waziwazi au kuyafumbata kwa methali.
Uchambuzi wa Ngano:
a) Wahusika- ni nani?
- ni watu au nu wanyama?
- Kama ni wanyama, wanawakilisha nini?
- Wahusika muhimu ni wapi?
- Wahusika wana sifa gani?
- Wanyama wanawakilisha sifa gani za binadamu?
b) Muundo au msuko:
- kuna nini mwanzo, kati na mwisho?
- Matukio yanahusiana kwa jinsi gani?
- Tukio gani linalosababisha matendo ya ngano?
- Kuna tatizo kuu?
c) Taharuki:
- hamu ya kusoma au kuisikiliza inatokana na nini?
- Hamu hiyo inakidhiwa mwishoni?
- Kama inakidhiwa, inakidhiwa kwa jinsi gani?
d) Maudhui:
- Ngano inahusu nini?
- Ujumbe mkuu unaopatikana ni upi?
e) Adili/ Maadili/ Funzo:
- ngano hiyo ina funzo gani?
- Inalenga kutuonyesha nini?
f) Dhamira:
- mwenye ngano alilenga kutuonyesha nini? ( lengo la mtunzi au mtambaji)
<<Ukurasa wa Kwanza <<Ukurasa
wa Pili
|
|