MSAMIATI...  Visawe  
l
 


   >>Isimu Jamii
   >>Semi za Jozi




 
Msamiati ni maneno ambayo huwa yanakanganya au kuleta utata yanapotumika katika
mazungumzo ya kawaida.

Tunaanza kwa Kuangazia Msamiati wa watu na vitu wanavyohusiana navyo

Kawaida        Msamiati
Mtu                      Adinasi, mja, insani, binadamu, insi, mahuluki, mudu
Mzazi:                  mvyele,
Mtoto                   mwana, (daka la mwana)
Baba                   abu,
Mama                  nina, nyoko
Mjomba               hau, khali
Shangazi             mkaza mjomba, mbiomba, halati
Binamu:               mkoi, bintiamu,
Msichana             Banati, gashi, binti , biti
Mvulana               mvuli
Kijana                  Shababi, kijulanga,
Kijana(mvulana)    Ghulamu,
Msichana mrembo        Kipusa, kisosho, mtotoshoo(mrembo zaidi-mrembo wa kani
Mwanamke mzeee        Ajuza, bikizee
Mwanamume mzee       Shaibu, buda,
Rafiki                            Mwendani, sahibu, nemshi, mwandani, somo, msiri, mbasi
Mtu mbaya                    mtu mui,
Mwanafunzi                   mwanagenzi
Mvuvi                           mwanapwa
Mwizi mdogo                pwagu
Mwizi mkuu                   pwaguzi
Maskini                         fukara, fakiri, mkata, hawinde, suta, mtule, mfilisi
Tajiri                             mkwasi
Mwanamke                  nisai
Mwanamume                ririali
Mwana wa kiume          dhukuria, auladi
Mja safi                         mtanashati, mfua uji, mlibwende,
Familia                          aila,
Ndoa                             nikahi, nikakaha
Zama za kale                 ndemi na mathathi, lela ulela, jadi na asili
Subira kwa hamu kuu      kwa hamu na ghamu, kwa raghba ya mkaja
Chakula                         riziki au kuti
Kiamsha kinywa             staftahi, kisebeo
Chakula cha mchana      kishuka
Chakula cha jioni            kilalio, chajio au kijio
Birika                             kandarinya
Damu                             ngeu, ng’eu
 

 


Haki zote zimehifadhiwa. Kunakili Makala yoyote kutoka Kwenye Tovuti Hii Bila Idhini Iliyoandikwa na Wakurugenzi Hakuruhusiwi. Makala yote yanamilikiwa na Gskool.com punde tu yanapotumwa.
Tuma Mchango wako
au maswali kwa kiswahili@gskool.com.
Home
  Legal  Contacts  Faqs    

©Gskool Educational Site