|
Tafadhali anzisheni kitengo cha methali,
misemo, vichekesho na vitendawili. Nitafurahia
sana kusoma haya katika gskool. -Victor |
|
Asante sana kwa mchango. Vitengo hivi tutavianzisha hivi karibuni. |
|
Ninaudhishwa sana na vile lugha za sheng'
na kimombo zinavyowaathiri wanafunzi. Ninawahimiza wanafunzi wote
wazingatie kwa makini utumizi wa lugha sanifu ili kuimarisha ufasaha
katika lugha ya Kiswahili la sivyo lugha ya Kiswahili, japo ni lugha
yenye asili yake katika eneo letu la Afrika mashariki, itakuwa kama
lugha yoyote ile ya Kigeni. -Jaccy (Statoe) |
|
Yangu si mawaidha mbali
pongezi kwa kazi nzuri mnayoendelea kufanya. Endeleeni vivyo hivyo
na bila shaka mtafikia upeo mwa juu Zaidi.......Bonnie |
|
Shukrani Bonnie, tutazidi kujikakamua |
| Sijui
kwanini kitabu cha walenisi kiliondolewa kutoka kwenye
silabasi. Ningetaka kuihimiza wizara ya elimu kukirejesha kitabu
hicho kwani kilikuwa kikifunza maadili ya jamii kwa wanafunzi
na kwa umma kwa jumla. Kilinipindua mimi na kingewanzindua wengi.
Steve (Nairobi) |
| |
|
Je,
muundo wetu mpya unakupendeza? Mcheza kwao hutuzwa... Tupe maoni
yetu kuhusu muundo wetu mpya. Shukurani. |
|
Tuma mawaidha yako
na maoni yako kwa
kiswahili@gskool.com |