Lugha  
l
 


>>
Ukurasa wa 1
>>Ukurasa wa 2
 
 

 

Chumba cha Majadiliano>>>  Tuma Maswali/majibu>>>

Lugha ya kiswahili ni lugha pana na itachukua muda usio mfupi kuieleza katika tovuti yetu. Hata hivyo tutajikakamua kutoa maelezo kwa mapana na marefu kuhusu vipengele muhimu katika lugha ya Kiswahili.

VIPENGELE MUHIMU VYA LUGHA:

NOMINO:
Ni neno linalotaja mtu, kitu, mnyama, kiumbe, mahali au hali fulani.

Aina za Nomino:
1. Nomino za pekee:- Mwendwa, Mombasa, Jumatatu, Athi, Ulaya, Machi, n.k.
2. Nomino za kawaida au jumla:-kisima, ndege, mtoto, kikombe, n.k.
3. Nomino za jamii:-bunge, kamati, jamaa, halaiki, kikosi, kwaya.
4. Nomino za wingi:- maji, maziwa, mate, mahubiri, makao.
5. Nomino dhahania:- utani, urembo, werevu, shetani, malaika, miungu.
6. Nomino za kitenzi-jina: -kutoroka, kukimbia, kuimba, kuabudu, kutafakari.

VIWAKILISHI (VIBADALA)
 Huchukua nafasi ya nomino-husimamia nomino.

Aina za Viwakilishi:
a) Viwakilishi vionyeshi (viashiria)  ...Hivi ni viwakili vinavyoonyesha mahali kitu au mtu alipo. Kwa mfano:
- Huyu ataondoka kesho.
- Hicho kitapelekwa kwa seremala.
- Lile lilifuliwa jana.

b) Viwakilishi virejeshi: ...Hivi ni viwakilishi vinavyrejelea mtu, kitu au jambo fulani. Kwa mfano
- Ambaye atakuja atalakiwa.
- Uhitajikao ni kweli.

c) Viwakilishi viulizi: ...Hivi hutumika katika kuulizia jambo fulani. Kwa mfano:
- pi? Nani?
- -ngapi? Lini?
- Gani? Nini?

d) Viwakilishi vimilikishi:  ...Hivi huonyesha umilikaji wa kitu fulani hasa vikirejelea mmiliki Kwa mfano:
- -angu -etu
- -ako -enu
- -ake -ao

e) Viwakilishi vya pekee:   ...Mifano ni kama ifuatayo:
- -enye -ingineo
- -enyewe -ote
- -ingine -o-ote

f) Viwakilishi nafsi:    Kuna iana mbili za viwakilishi nafsi:
viwakilishi nafsi huru
mimi sisi
wewe nyinyi
yeye wao
viwakilishi nafsi viambata
Amefungwa kwa kuwatesa watoto.
Mmewalaumu bure.

VITENZI:
Hueleza tukio lililofanyika au litakalofanywa na mtu, mnyama au kimbe.

Aina za Vitenzi:
a) Vitenzi halisi:- huarifu kuhusu:
- tendo linalotendeka- lima
- wakati wa kutenda jambo- analima (uliopo)
- hali ya kitenzi- amelima (timilifu)- angalifika (ya masharti)
- kauli ya kitenzi- anapika (kutenda)- wanapikiana (kutendeana)
- uyakinishi au ukanushi- anasoma (uyakinishi)- hasomi (ukanushi)

b) Vitenzi vikuu (T):- hueleza lililofanywa, mtenda na labda mtendewa k.m. Mgeni aliwatembelea wenyeji.

c) Kitenzi kisaidizi (Ts):- husaidia kitenzi kikuu kuleta maana kamilifu k.m. Muchiri alikuwa (Ts) anachapa (T) mswada.

d) Kitenzi kishirikishi (t):- huonyesha tabia au hali iliyopo au isiyokuwepo kihali, kitabia na kimazingira k.m.
- Onyango ndiye shujaa.
- Savalanga yu kambini.
- Mueni si mjinga.

i) vitenzi vishirikishi vikamilifu-huchukua viwakilishi nafsi au viambishi ngeli au viambishi vya wakati k.m. Wao walikuwa wangapi mchezoni?

ii) Vitenzi vishirikishi vipungufu- havichukui viambishi vya wakati ingawa vinaweza kuchukua viwakilishi nafsi au viambishi ngeli, navyo ni: si, ni, ndi.k.m.
- Yeye ndiye mkuu.
- Wao si watu wa kutegemewa.
- Mimi ni mkuu wa idara hii.
Wewe u mtu wa ajabu sana.

e) Vitenzi Sambamba:- ni vitenzi ambavyo hutokea mfululizo k.m. kitenzi halisi na kile kishirikishi au kisaidizi, kitenzi kisaidizi na kile kikuu k.m.
- Maina angali (t) anasoma (T).
- Nyakweba alikuwa (ts) akienda (ts) kuwinda (T).
- Wewe utakuja (ts) kujuta.

Waweza kutuma mengi kuhusu lugha kwetu na waweza kuwa mshindi wa tuzo letu
Huu ndio mwanzo. Endelea kusoma makala zaidi upate umaarufu.

 


Haki zote zimehifadhiwa. Kunakili Makala yoyote kutoka Kwenye Tovuti Hii Bila Idhini Iliyoandikwa na Wakurugenzi Hakuruhusiwi. Makala yote yanamilikiwa na Gskool.com punde tu yanapotumwa.
Tuma Mchango wako
au maswali kwa kiswahili@gskool.com.
Home 
Forums and Discussions  Legal  Contacts  Faqs

©Gskool Educational Site