|
16. Kwa kuigiza kama mhusika Mwelusi ukiwa gerezani, mwandikie mamako
barua ukimweleza matatizo unayoyapata humo.
(alama 20)
17. Ukaragosi ni ili hali
ya kutumiwa na watu walio mamlakani kutimiza matakwa yao bila kujali
madhara yanayowapata watu wengine.Eleza jinsi vikaragosi wametumiwa
kufanikisha uongozi wa Bokono.
(alama 20)
18. Mataifa jirani ya
Butangi yameitisha mkutano kujadili kuhusu lawama wanayotwikwa na Bokono
kuhusu vita vya wenyewe kwa wenyewe katika sehemu fulani ya Butangi.
Ukiwa katibu wa mkutano huo, andika kumbukumbu zote, ukilenga hisia za
wahusika na maamuzi yao.
(alama 20)
19. Maendeleo ni ya
wachache na dhuluma ni kwa wengi wasiojiweza. Tetea na upinge kauli hii
ukizingatia tamthilia ya Kifo Kisimani.20
20. “ Nilikuwa nafikiria
pengine kuna jambo ambalo lilikuwa linakusumbua moyoni.Ikiwa lipo,
niambie. Usinifiche mimi ni mkeo, mwandani wako, msiri awko.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hii.
(alama 4)
b) Eleza yanayotokea baadaye hadi hatima yake.
(alama 10)
c) Eleza umuhimu wa anayezungumaz tamthiliani.
(alama 6)
21. “ Ni kweli naota.
Naota daima. Naota juu ya Butangi.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hii.
(alama 4)
b) Taja mambo yoyote saba ambayo anayezungumza aliyaotea.
(alama 7
c)Taja mambo mabaya mzungumzaji anayataja na yanayoonyesha ni kwa nini
anaupendelea uongozi wa Mtemi Mlima. (alama 7)
d)Kulingana na mzungumzaji, maua ya kazi yao yalichanua mna kupamba
mandhari ya Butangi. Toa sababu yako. (alama 2)
22. “Hatuko watatu.
Wanabutangi ni wengi. Watakomboa Kisima cha Mkomani.Watakomboa
Bonde la Ilangi.”
a) Eleza muktadha wa maneno
haya. (alama
4)
b) Eleza vile Gege
alivyofaulisha mpango wake kwa kumuua Mwelusi. (alama5)
c) Je, wanabutangi
walipaswa kuteka maji wapi kulingana na kanuni za Butangi?
(alama 1)
d) Eleza sifa na tabia za
mzungumzaji. (alama 10)

23. “Uongozi kwa Mungu,
mamlaka yangu yametoka juu. Mungu aliniketisha kwenye kiti cha enzi cha
Butangi. Alifanya....kwenye kiti cha Mtemi.”
a) Eleza muktadha wa maneno
haya. (alama
4)
b) Dhibitisha kuwa uongozi
wa Bokono haukutoka kwa Mungu kama yeye anavyodai.
(alama 16)
24. “Kwamba tumetoka tumbo
moja haimaanishi una ruhusa ya kunitusi vivi hivi.Naweza kukufanya jambo
ukashindwa kujua kama ni mchana au usiku.”
a) Eleza muktadha wa dondoo
hii. (alama 4)
b) Onyesha vile usemi
huu ulikuja kutimilika.
(alama 10)
c) Eleza sifa na tabia za
anayezungumza. (alama 6)
25. “Manung'uniko juu ya
mambo madogo madogo. Kwa mafno, baadhi ya watu wanasema kwamba
wananyimwa haki ya kutumia maji ya kisima.”
a) Eleza muktadha wa dondoo
hii. (alama 4)
b) Eleza sifa bna tabia za
anayezungumza. (alama 10)
c) Onyesha vile mchochezi
alivyoadhibiwa. (alama 6)
26. Tamthilia ya Kifo
Kisimani haijapitwa na wakati. Jadili. (alama 20)
27. 'Kifo Kisimani'
ni anwani mwafaka kwa tamthilia hii. Jadili.
(alama 20)
28. Eleza kwa undani
tasnifu ya ujumbe unaojitokeza kwenye jalada la kitabu cha tamthilia ya
Kifo Kisimani. (alama 20)
29. Uongozi wa kiimla wa
Mtemi Bokono ulitegemea usaidizi kutoka kwa watu wengine ili kuweza
kufua dafu na kuuendeleza. Jadili kauli hii huku ukitolea mifano mwafaka.
(alama 20)
30. Huku ukiirejelea
tamthilia hii ya Kifo Kisimani, linganisha uongozi wa Mtemi
Mlima na Mtemi Bokono. (alama 20
<<<Rudi Nyuma
|