1. Uovu wa uongozi katika
nchi zianazokua umejikita barabara katika tamthilia ya Kifo Kisimani.
Thibitisha.
(alama 20)
2. Maudhui ya utu na wema
yametanda kote katika tamthilia hii ya Kifo Kisimani.
Thibitisha. (alama
20)
3. Eleza sifa na hulka za
wahusika wafuatao:
a)
Bokono
b)
Mwelusi
c)
Tanya
d)
Nyalwe
e)
Batu
4. Wanawake wamepewa nafasi
kubwa katika jamii hii ya Kifo Kisimani. Jadili huku ukitolea
mifano mwafaka.
(alama 20)
5. Eleza mbinu hizi za
uandishi na lugha kama zilivyoweza kujitokeza katika tamthilia hii:
a)
Ndoto/ ruia
b)
Mbinu rejeshi/
kisengerenyuma
c)
Utabiri/
ubashiri
d)
Jazanda
e)
Istiari
f)
Sadfa
6. Taja mambo manne
anayoahidiwa Mwelusi na Batu endapo atauunga mkono uongozi wa Mtukufu
Mtemi
Bokono. (alama4)
7. Je, Mwelusi angependa
Butangi iwe vipi? (alama 10)
8. Maudhui ya usaliti
yanajikita barabara katika tamthili hii ya Kifo Kisimani. Jadili.
(alama 20)
9. Thibitisha, kwa kutolea
mifano jinsi mbinu zifuatazo zilivyotumika katika tamthilia hii:
a)
Methali
b)
Kinaya
(alama 20)
10.Kwa kuzingatia matukio
katika tamthilia ya Kifo Kisimani ya Kithaka wa Mberia, fafanua
kwa kutolea mifano nafasi ya mwanamke ukirejelea vijana na wazee. (al.
20)
11. Onyesha kwa kuzingatia
matukio ya Kifo Kisimani ukombozi unavyojitokeza na jinsi mataifa
ya Afrika yanaweza kujikomboa. (alama 20)
12. Kwa kuigiza kama
mhusika Mwelusi andika hotuba yenye angalau sababu kumi kwa nini
ungependa msaada wa Wanabutangi kumng’oa Bokono mamlakani. (al. 20)
13. “...Njiwa na Kozi ni
ndege wenye maisha tofauti. Tungalikuwa sote njiwa au sote kozi,
ningalikuelewa vyema zaidi. Tungalikuwa na tabia zilizolingana,
ningalikuelewa zaidi sana.”
a)
Eleza
muktadha wa dondoo hii. (alama 5)
b)
Ni nini
dhumuni la nayezungumziwa kumjia mzungumzaji? (alama 3)
c)
Taja na
ueleze sifa tatu tatu za:
i)
Mzungumzaji
ii)
Mzungumziwa
(alama 6)
d)
Eleza jinsi
mzalendo kati ya wahusika katika swali la (c) anavyooshesha uzalendo
wake. (alama 6)
13. Linganisha matukio ya
kisiasa katika mataifa ya Kiafrika na mtiririko wa mawazo katika
tamthilia ya Kifo Kisimani. (alama 20)
14. Kulingana na tamthilia
ya Kifo Kisimani, usaliti unajitokeza mara kwa mara . Kwa kutoa
mifano mwafaka, onyesha jinsi maudhui haya yanajitokeza. (alama
20)
15. X: Hujambo, Mtukufu
Mtemi wa Butangi...
Mtemi haongei.
Ulimfanya nini.
Y: Sikumfanya
lolote baya.
X: Hebu jaribu
kukumbuka.
Y: Nakumbuka vizuri.
Sikumafanyia kosa lolote....
a)
Eleza muktadha wa dondoo hii. (alama 7)
b)Taja na ueleze mbinu
iliyotumiwa katika dondoo hii. (alama 3)
c)
Taja sifa
mbilimbili za:
i)
Mhusika X
ii)
Mhusika
Y (alama 6)
iii)
Mhusika
anayezungumziwa
d)
Eleza jinsi
mhusika anayezungumziwa anachangia katika kufanikisha maudhui makuu ya
Kifo Kisimani. (alama 4)
Maswali
Zaidi>>>
|