Mwangaza- Toleo la 14  
 
Maswali
Mabingwa
Jarida
Tuzo Letu
Mawaidha
Methali
Kamusi

Kukuru Kakara za Mwaka
Manabii wa Uwongo
Ukweli
Bustani la Kuzimu
Nasaha
Jina Bora
Uchambuzi wa Ushairi
Dosari Duniani
Mwaka Wetu mpya 2007
Muundo mpya wa www.gskool.com
Mashairi Yetu

Nasaha...  Na Alfonce Nzioka
 

Chonde chonde wapenzi wa Kiswahili. Karibuni nyie mnaoenzi na kustahi lugha hii tukufu yenye kunoga na kuhomolewa. Njooni tuseme mawili matatu kwa pamoja kwani heri nusu shari kuliko shari kamili. Yakini wala si yamkini kuhimarisha Kiswahili ni jambo alaa na aula. Tena ni wajibu wetu ambao hatufai alaa kulihali kuupuza. Ni dhima yetu tukufu kuhakikisha kuwa umufti na usanifu wa Kiswahili umechupa juu na kupita mipaka. Waama, hicho kitakuwa Kiswahili cha kufurahisha kupendeza na kutamaniwa. 

Bila shaka, abezaye Kiswahili ni hasidi wa mustakabali wake kwani Kiswahili ni kurunzi ya maisha imulikayo kwa mwangaza unaomwayamwaya na kumeremeta metumetu.Apendaye maisha yake hana budi kuishikilia kurunzi hiyo kikiki, mathalani kugandana nayo kama kupe na mkia wa mbuzi. Dhahiri shahiri, kurunzi hiyo ikianguka au kupotea insani yeyote hana budi kusepetukasepetuka, haoni mbele wala nyuma. Kwa nini mja kumtafuta paka mweusi tititi kwenye kiza totoro?  

Kudhalilisha na kudunisha Kiswahili ni sawa na chachandu aliyejipalia makaa. Ama kwa hakika, anayedharau Kiswahili huwa anajipachika misimbo, anajipaka mashizi mwenyewe. Chambilecho wahenga na wahenguzi, ibilisi wa mtu ni nafsi  yake.  

Hatufai kukinai na kuridhika na kitembo cha Kiswahili tulicho nacho bali tufanye utafiti wa kina  bila kuregea regerege kama utumbo wa samaki, au la mboga ya mayugwa. Ajitambazaye kwa mapana na marefu akidai na kujidai kuwa anajua sana ni kama debe tupu ambalo daima haliachi kutika. Waama, akili nyingi huondoa maarifa. Tujifunge mkaja katika kujiendeleza katika ufahamu wa Kiswahili hadi tuwe wataalamu waliotaalamika katika taaluma mbalimbali za lugha. Kweli, atafutaye hupata akikosa hastahili kupata, kama anadivyo msanii mbobeaji, Alfonce Nzioka

Mwanzo wa jarida  Mwanzo wa Kurasa za Kiswahili

 


Haki zote zimehifadhiwa. Kunakili Makala yoyote kutoka Kwenye Tovuti Hii Bila Idhini Iliyoandikwa na Wakurugenzi Hakuruhusiwi. Makala yote yanamilikiwa na Gskool.com punde tu yanapotumwa.
Tuma Mchango wako
au maswali kwa kiswahili@gskool.com.
Home 
Forums and Discussions  Legal  Contacts  Faqs

©Gskool Educational Site