| |
Kukuru Kakara za Mwaka
Manabii wa Uwongo
Ukweli
Bustani la Kuzimu
Nasaha
Jina Bora
Uchambuzi wa Ushairi
Dosari Duniani
Mwaka Wetu mpya 2007
Muundo mpya wa www.gskool.com
Mashairi Yetu
 |
|
MWaka wetu mpya
2007
na Edwin Kimondo |
|
|
Hujambo msomaji?
Ninatumaini u hali njema na kuwa umeweza kuuanza mwaka wako kwa njia
inayofaa kabisa. Je, waweza kujiuliza kwa nini u hai siku ta leo?
Kwa nini u mzima hivyo?
Hebu chukua muda mfupi ufikiri na
utafakari kuhusu maswali haya ambayo kila binadamu anafaa kujiuliza.
Wenzangu mio shuleni mnasoma ili baadaye muyatimize yepi? Mnasoma
ili mmtumikie nani? Au ili muwe watu aina gani? Sitaki kubananga
wakati lakini nataka kuwaelezea kinaganaga kuwa tuliumbwa, tunaye
Mola ambaye ametuwezesha kufika tulipofika. Ndio maana tuka hai
mwaka huu na wazima kama vigongo. Basi kwa hivyo, twafaa kuelewa
kuwa mwaka huu ni wetu. Huu ndio wakati wako wa kufanya bidii;
utaishi mara moja tu. Elewa kuwa una uwezo, uzima wa kutekeleza
jukumu ulilopewa na mungu aliyekuumba. Unaishi kwa kuwa una jukumu
ambalo unafaa kutekeleza. Ni ombi langu kwa kila mmoja wetu kuelewa
analofaa kufanya mwaka huu ili mwisho wake utakapofika aweze
kufutarahia matunda ya juhudi zake. Kama wewe ni mwanafunzi basi
huna la ziada ila kutia bidii masomoni na kupasi vyema kwani lisilo
budi hubidi.Tuyasahau yaliyopita tuyagange yajayondo mwito wangu kwa
kila mmoja wetu. Hakuna wakati wa kutosha na tusipofanya uamuzi
wowote basi tutabaki kujilaumu wenyewe. Hakuna haja ya kuyapa majuto
nafasi, hivyo basi ni kheritujizatiti kweli kweli na tusisahau
kwamba tuna wajibu tuliopewa na tukiutimiza tutakuwa tumeleta furaha
kwake.
Kwa hitimisha, huu ni mwaka wetu ;
twafaa kuelewa kuwa wakati unazidi kupita na pindi si pindi itakuwa
Krismasi. Naam, tusiishi kama wasiojifahamu. Tunaye Rabuka wa
kutuelekeza katika hekaheka zetu zote.
JOPO LA KISWAHILI LAWAOMBEA NYOTE UFANISI MWAKA HUU MPYA!
Mwanzo wa jarida
Mwanzo
wa Kurasa za Kiswahili |
|
|