|
Tovuti ya kipekee nchini
inayoshughulikia maswala ya elimu katika kiwango cha shule za upili
sasa imepata muundo mpya. Haya ni kulingana na mkurungenzi mkuu Bw.
Mutevu. "Lengo letu kuu ni kuhakikisha kwamba kila mwanafunzi hasa
hapa nchini na ulimwenguni kote kwa jumla amepata elimu bure bilashi."
Alisema.
Tovuti ya gskool.com ina vitengo mbali
mbali ambavyo vinashughulikia maswala tofauti tofauti.
Kunacho
kitengo cha wiki ambacho
muundo wake ni kama ule wa wikipedia.com. katika kitengo hiki,
unaweza kuanzisha makala yako au kuruwaza makala yaliyochapishwa na
mtu mwingine. Makala yote yaliyochapisha katika kitengo hiki huwa
hayana haki zozote za kuhifadhiwa.
Kitengo cha Forums(majadiliano)
hushughulikia majadiliano baina ya wasomaji wa makala yaliyomo.
Msomaji anaweza kuandika swali na kuwaachia wasomaji wengine kutoa
jibu. Pia anaweza kutoa jibu au wosia kwa wasomaji wengine. Katika
kitengo hiki, utapata mengi kuhusu masomo mbali mbali, makala ya
walimu, marafiki, na kadhalika.
Kunavyo vitengo vingine ambavyo
utavipata katika tovuti hili.
Kiswahili
Gskool imejikakamua vilivyo kuimarisha
kiswahili kwani ni nadra sana kupata tovuti ya kiswahili. Kurasa za
kiswahili zimeundwa kwa kuzingatia sehemu muhimu za kiswahili kama
vile fasihi, ushairi, lugha, insha na kadhalika. Mkuu wa idara ya
kiswahili alitufahamisha kwamba hivi karibuni kuna nia ya kuanzisha
kamusi ya kipekee...
Habari njema kwa wasomaji wa mwangaza
ni kwamba sasa mtaweza kuyapata baadhi ya makala tuyachapishayo
katika jarida letu la mwangaza katika kitengo cha jarida katika
sehemu ya kiswahili (www.kiswahili.gskool.com/jarida).

Mwanzo wa jarida
Mwanzo
wa Kurasa za Kiswahili |