Jina
zuri bila shaka ni bora kuliko asali tamu. Ndio ni bora hata zaidi
ya mafuta ya kupendeza
yenye mvuke wa kuvutia. Kitabu kitakatifu cha Mungu kinatuelezea
haya kinaganaga.
Aidha ningependa kuongezea kuwa jina duni ni baya kuliko harufu ile
mbovu zaidi ulimwenguni.
Walakini ningependa
ufahamu kuwa jina zuri si jina tu la mtu binafsi bali hisia nzuri
zinazuka miongoni mwa waja wengine jina lako linapotajwa. Aghalabu
katika akili ya mwanadamu, lazima kutajwa kwa jina fulani kunazua
hisia fulani mwilini. Swali ni je, watu wanaposikia kukuhusu
hufikiria nini kwanza? Je, wao huona mjinga, mwizi, mlaghai, mkora,
kahaba na kadhalika au huona mtu utu mwenye utu, mtiifu, mwenye nuru,
anayeweza kuaminika au vipi?
Tunaweza kujipatia majina mazuri si kwa kuwaambia watu au
kujisifu mbele ya wenzetu
bali kwa vitendo vyetu sisi wenyewe. Mja aamuapo kutii na kutekeleza
jikumu lake
hali kadhalika kufanya mema zaidi ya anavyopaswa, huyo hujiwekea
msingi imara na dhabiti usioweza kutingizika kamwe. Mwenye jina bora
zaidi atajipatia heshima zake mwenyewe na aila yote ya watu
itatambua mema yake na kumlipa ipasavyo. Kadhalika, kuna tofauti ya
jina zuri na jina linalojulikana na wengi. Ni kweli wengi wanaweza
kukujua lakini kwa mabaya wala si mazuri yako. Hapo basi wakikuona
watakukinai. Unapotoa hoja haitaungwa mkono.
Kuanzia mle vitongojini,
unapaswa kutia imani mioyoni mwa wanakijiji, aila yako na wenzako
kuwa wanaweza kukuamini kwa lolote lile. Wao watakupenda na zaidi ya
yote watakuthamini kwa lolote lile. Wakati wa dhiki watakuauni kwa
sababu ya jina zuri ulilojitafutia mle kijijini. Iwapo kuna msako
fulani, ninakuhakikishia kuwa hautakuwa miongoni mwa washukiwa.
Vivyo hivyo, utaendelea kufurahiya neema yako katika Bwana.
Vilevile, hapa kwetu skulini, wanagenzi wanaweza kuweka
msingi dhabiti baina yao
na viranja. Hii inawezekana tu ikiwa kila mmoja kama
nilivyotanguliza atafanya
majukumu yake bila kulazimishwa wala kukumbushwa. Wa aidha, sio tu
kutekeleza bali kuifanya katika hali inayofaa zaidi. Si kwa kuogopa
adhabu bali kwa kuwa ni jambo linalostahili. Unapofanya hivyo, hata
viranja wenyewe watakupa heshima unayostahili. Hii ni kumaanisha
kuwa hautakuwa na wakati mgumu na viranja. Ikiwa utaepuka makaosa,
na kama umepatikana na kuso lolote kuchukulia adhabu unayopewa kama
marekebisho, na kuifanya bila kulalamika, basi utakuwa katika upande
ufaao. Ni viranja haba ambao watapania kukufuata tu bila sababu.
Walakini ukitaka kuwaonyesha kuwa unajua kutetea haki zako, basi
utaumia.
Kwa kujitafutia jina
zuri miongoni mwa viranja, viongozi wako, walimu na kadhalika
unajiongezea neema kadha wa kadha. Unapotaka kukata rubani kwa kesi
yoyote ambayo unafikiri uliadhibiwa kimakosa, utasikizwa. Kwa kuwa
haujakuwa ukihusika na makosa kama hayo, watakuamini na hata kama
umekosa, utawiwa radhi. Lakini kwa wenye majina yaliyokolea uchafu
na dosari hata kama hawajakosa itakuwa hawana kosa lolote, huenda
wakaadhibiwa tu kwa sababu wamehusika sana na vitendo haramu.
Hawataaminika katu. Ole wao! Wataonekana kuwa wanadanganyifu na
masaibu yatawafuata. Kwa sababu ya jina baya.
Kwa yakini kila mtu
atakuamini na ndiposa hata kitendo kinapotendeka hutakosa kusikia
waja wakisema, " Najua fulani hawezi kufanya jambo kama hilo" ama "Kama
ni fulani, sina shaka kamwe, mambo yote yatakuwa shwari." Si kwa
kuwa wana ushahidi wa kutosha kuwa ni kama wanavyodhania bali tu kwa
asbabu ya jina lako ulilojitafutia.
Kaditamati, Mashoga wangu ningependa
kuwapa nasaha yenye busara kuhusu uchaguzi wako wa kuteua jina bora
au baya. Wakati ni sasa. Usibanange mwia zaidi. Chagua jina zuri leo.
Utapanda mbegu nzuri na mavuno yake ni ya kuridhisha.