ISIMU JAMII  
l
 


>>
Isimu Jamii
>>Semi za Jozi


 


 

 

Chumba cha Majadiliano>>>  Tuma Maswali/majibu>>>
UTANGULIZI
Kufuatana na mfumo wa silabasi mpya uliowekwa na Taasisi ya Elimu ya Kenya ili kuimarisha na kuendeleza lugha ya Kiswahili baina ya wasomaji na wazungumzaji, kulipitishwa kuwa kipengele cha isimu –jamii kirudishwe tena katika somo la Kiswahili. Hiki ni kipengele ambacho zama za zama kilikuwa kinafundishwa shuleni na hata vyuoni lakini kwa sababu moja au nyingine, kikawekwa kando. Kurudishwa tena kwa kipengele hiki cha lugha katika silabasi mpya ni jambo murua na la kujivunia sana hasa tunapozingatia kuwa mwacha mila ni mtumwa na pia kuwa hii ni njia mojawapo ya kuonyesha na kudhihirisha kukua kwa lugha kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Hata hivyo, jambo hili limewawia kizungumkuti mahuluki lukuki madhali isimu jamii ilikuwa imetupiliwa mbali  katika kaburi la sahau. Iliyokufa fo! Habari njema ni kuwa, hakuna refu lilsilokuwa na ncha kwani uozo huo umefikia kikomo.Itakuwa ni dhambi kama si kosa au hatia nisiposhughulikia baadhi ya istilahi au msamiati unaotumiwa katika lugha ili kuiondoa siutafahamu iliyoko kuhusu maneno anuwai na pia ili kukuangazia wewe msomaji upevuke juu ya yale unayoyasoma.  

Isimu (linguistics)—ni mtalaa ambao huchunguza, huchanganua na pia kuchambua na kufafanua lugha kama
       mfumo wa mawasiliano baina ya wanadamu.

Isimu-Jamii—ni mtalaa unaochunguza lugha ikiwa katika muktadha wake wa matumizi na wanaoitumia –jamii.

Lugha -- ni mfumo wa mawasiliano  unaotumia mpangilio maalum wa sauti kuunda vipashio vikubwa zaidi k.m.
        mofimu, neno, sentensi n.k. Ni mfumo wa sauti ishara na masolugha.

Lahaja—haya ni matumizi tofauti ya lugha moja kulingana na mazingira ya mzungumzaji.

Lafudhi—haya ni matamshi au namna ya kutamka maneno katika lugha fulani.

Lugha ya Taifa—lugha inayotumiwa kuwatambulisha na kuwaunganisha wananchi wa nchi au jamhuri fulani  ili
       kuweza kutambulika na pia kuendeleza muiano na utangamano.

Lugha sanifu—hii ni lugha ambayo imefanyiwa marekebisho na ukarabati anuwai ambapo wanaoisanifisha
       huafikiana kuhusu vipengele mbalimbali.k.m. Fonimu, Mofolojia, Sintakisia, semantiki na msamiati.

Lugha rasmi—ni lugha inayoteuliwa katika nchi fulani ili kutumiwa katika mawasiliano yaliyo rasmi katika nchi
       husika k.m. Kiingereza.

Lugha rasimi—huwa ni mtindo fulani wa lugha hasa uliotumiwa zamani na watu mashuhuri na ukaaminika kuwa
     
 kuwa ni mtindo bora wa lugha unaofaa kuigwa na wengine. K.m.  ule uliotumiwa na William Shakespeare,
       Kigiriki, n.k.

Lugha mame—hii ni lugha ambayo bado haijakua na imo katika umbo lake la awali.

Lugha azali—hii ni lugha ambayo huzaa lugha zingine au nyingine.

Misimu—ni lugha ya kisiri ambayo hutumiwa na kikundi fulani cha watu katika jamii k.v. kwa kutumia mafumbo au
        lugha –simo (Sheng’)

Pijini—hubuniwa kwa kukopa msamiati kutoka lugha mbalimbali ili kutumika kwa mawasiliano baina ya watu
      ambao lugha zao ni tofauti na hawana lugha moja wanayoielewa.

Krioli—ni lugha ambayo hutokana na pijini kukua, kukomaa , kupevuka na kuendelea.  

Baadhi ya sajili za lugha ni kama vile: Lugha ya Mahakamani, Dini, Sokoni, Magazetini, Mahojiano, Simu, Wanahirimu, Wataalamu, Majambazi, Hospitalini, Mapenzi, Michezoni, Utambaji, Matatu, ya Taifa, Biashara, Mazishi-Matanga, Kawaida, Wanasiasa, Ofisini, Wazee, n.k..

Kwa makala zaidi kuhusu sifa na mifano ya sajili au rejista mbalimbali za lugha, jinunulie nakala yako ya kitabu cha ‘Nuru ya Isimu Jamii-Na David W. Ndegwa’,aliye Mlezi wa Jopo la Kiswahili la Shule ya Upili ya Starehe na pia mwalimu aliyebobea katika Lugha Tukufu ya Kiswahili shuleni mumo humo.

 


Haki zote zimehifadhiwa. Kunakili Makala yoyote kutoka Kwenye Tovuti Hii Bila Idhini Iliyoandikwa na Wakurugenzi Hakuruhusiwi. Makala yote yanamilikiwa na Gskool.com punde tu yanapotumwa.
Tuma Mchango wako
au maswali kwa kiswahili@gskool.com.
Home 
Forums and Discussions  Legal  Contacts  Faqs

©Gskool Educational Site