|
Chumba cha Majadiliano>>>
Tuma Maswali/majibu>>>
Insha ni utungo ambao kwa mara nyingi huwa ni maoni ya mwandishi. Kwa
mara nyingi, insha huandikwa kwa ajili ya mitihani lakini kumbuka kwamba
insha inaweza kuandikwa kama kumbukumbu ya matukio fulani mbila
madhumuni ya kutahiniwa.
Kwa kufuatia mfumo wa sasa wa elimu Nchini Kenya, kuna insha za aina
mbalimbali ambazo mwanafunzi anaweza kutahiniwa kama vile
- Insha za Kubuni
- Insha za Barua
- Insha za Hotuba
- Insha za "Kuendeleza Kifungu Fulani"
- Isha za kumbukumbu
- n.k
Katika uandishiwa insha mwanafunzi
anastahili kuzingatia mambo mbali mbali ambayo yanaweza kufanikisha
uandishi wainsha yake.
Kwanza kabisa tahajia lazima iwe ya
kuvutia na kupendeza. Hili huifanya insha kuweza kusomeka kwa urahisi
jambo ambalo huwafurahisha watahini wengi.
Pili mwanafunzi anastahili kuzingatia
maendelezo na kuhakikisha kwamba insha yake haina makosa yoyote ya
maendelezo. Isisahaulike kwamba kila kosa la maendelezo hutozwa alama,
hadi alama zifikapo tano.
Mfululizo wa mawazo pia ni jambo la
kuzingatia vilevile. Kusoma inha isiyo na mfululizo mwema ni kama
kuendesha gari katika baraste yenye mawe na visiki. Dereva hawezi
kufurahia kuendesha gari katika baraste kama hiyo na vivyo hivyo mtahini
hawezi kufurahia kusoma insha kama hiyo.
Isitoshe, mwanafunzi anastahili kuandika
insha akifuata mfululizo unaokubalika katika uandishi. Kwa mfano huwezi
kuandika barua rasmi ukitumia aya kama ilivyokuwa hapo awali.
Haya na mengine mengi yanastahili
kuzingatiwa ili kuhakikisha kwamba insha yenyewe ina ladha na bila shaka
huwezi kukosa kupata alama za juu.
Waweza kutuma insha yako
kwetu na kuwa mshindi wa tuzo letu
Endelea kusoma makala zaidi upate umaarufu.
|