| |
    
>>Kifo
Kisimani
>>Mwisho wa Kosa
>>Mayai Waziri...
>>Fasihi Simulizi

|
Chumba cha Majadiliano>>>
Tuma Maswali/majibu>>>
FASIHI NI NINI?
Fasihi ni sanaa ambayo wasanii wake huonyesha ustadi wao katika
kutumia maneno kisanaa ili
kuwasilisha ujumbe wao kwa wasomaji au jamii husika.
TANZU ZA FASIHI:
1. Fasihi Andishi- Hii ni fashi iliyoandikwa vitabuni.
Vipengele vyake ni:
a) Riwaya
b) Hadithi fupi
c) Tamthilia
d) Ushairi
2. Fasihi Simulizi- Hii ni aina ya fashihi ambayo hupitishwa
kutoka kizazi kimoja hadi kingine
kupitia neno la mdomo.
Tofauti baina ya Ngano/ hadithi fupi na Riwaya
i) Urefu
ii) Uchoraji wa wahusika.
iii) Uchoraji wa mazingira.
iv) Ploti- mtiririko/ mfululizo wa matukio.
Uchambuzi wa Hadithi fupi:
1. Maudhui- maswala yanayowakilishwa na hadithi fupi (hoja
kuu)
2. Dhamira- lengo kuu linalojitokeza la mwandishi
kuandika ngano hiyo.
3. Ploti- mtiririko wa matukio katika hadithi fupi (mwanzo,
mwili na hitimisho)
4. Mazingira- maudhui ki-wakati na ki-mahali ambayo
hadithi fupi imetokea.
5. Wahusika- viumbe vinaoshiriki au wanaoshiriki (binadamu,
milima, miti )
6. Tasnifu- wazo kuu analowasilisha mwandishi na
kulitetea (Kariha, msukumo, jadhba au jazba)
7. Hisi- jinsi kiumbe wa hadithi anavyoathiriwa na
mazingira k.m. furaha, huzuni.
8. Fani- mambo yanayofanywa katika kazi ya sanaa
kufanikisha uwasilishaji wa ujumbe.
Mifano ya Fani mbalimbali
i) Mbinu rejeshi (kisegerenyuma)- kurejelea na kutalii matukio
yaliyopita awali.
ii) Taharuki- kumweka msomaji katika hali ya mbabaiko kuhusu
litakalotendeka.
iii) Tamathali- matumizi ya mbinu kama misemo, tashhisi, tashbihi.
iv) Kilele- pale suluhisho la maswali msomaji anafanywa kujiuliza na
mwandishi linapopatikana
(Upeo wa juu)
v) Mtindo wa usimulizi- kutumia nafsi ya kwanza au tatu, kupiga chuku na
kutumia takriri.
vi) Muda- muda unaochukuliwa na hadithi.
Ukurasa Ufuatao >>>
Ukurasa wa Mwisho>>>
|
|